Hadi kufikia Alhamisi jioni ilipopigwa kura na Guinea/Mali kutupwa nje ya fainali hizo za 30, timu hizo mbili zilicheza mechi tatu, zikatoka sare ya 1-1 dhidi ya Ivory Coast, Senegal na Cameroon.
Kwa matokeo hayo, timu hizo mbili zilikuwa na pointi tatu, mabao matatu ya kufunga, kufungwa, jambo ambalo limezua maswali mengi.
Ni bahati mbaya kuona timu mojawapo kati ya hizo ikirejea nyumbani mapema kwa sababu ya kanuni.
Ni matokeo ambayo hayakutarajiwa na wengi, isipokuwa yameamuliwa kwa kanuni za Shirikisho la Soka la Afrika (CAF)
Zinasemaje kanuni za CAF:
- Kwamba, inapotokea pointi hazitoshi kutoa mshindi, yataangaliwa matokeo baina ya timu mbili zinazohusika.
- Baada ya hapo, tofauti ya mabao yaliyofungwa itaangaliwa na kila timu
- Endapo timu bado zimelingana hadi mwisho wa makundi, kuna njia moja, itapigwa kura ambayo itasimamiwa na kamati ya maandalizi.
Kwa maana hiyo, matokeo ya kundi zima yangeweza kuamuliwa kwa kura, kama mchezo wa mwisho ungemalizika kwa sare inayofanana, yaani baina ya -- Ivory Coast vs Cameroon, kama ilivyofanyika kwa Mali vs Guinea. Kwa mfano, kama matokeo yangekuwa Ivory Coast 2-2 Cameroon na Mali 2-2 Guinea.
Hata hivyo, endapo mchezo mmojawapo ungekuwa na sare ya mabao mengi zaidi kuliko mwingine, kura ingefanyika kuamua ni timu gani ichukue nafasi ya kwanza. Kwa mfano, kama matokeo yangekuwa, Ivory Coast 2-2 Cameroon na Mali 1-1 Guinea, basi Ivory Coast na Cameroon zingefuzu kwa idadi kubwa ya mabao, lakini kura ingepigwa kuamua nani mshindi wa kwanza.
Vinginevyo, endapo mechi mojawapo ingemalizika kwa sare na nyingine kwa matokeo mazuri kwa timu moja, kama ambavyo imetokea baina ya Ivory 1-0 Cameroon na Mali 1-1 Guinea, kura ilikuwa lazima baina ya Mali na Guinea ili kupata timu ya pili ya kuunga na Ivory Coast.
Post a Comment