Timu ya taifa ya Ivory Coast imetwaa kombe la mataifa ya Africa baada ya kuifunga Ghana kwa penalt i9-8 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120 katika mchezo ulifanyika katika uwanja wa Bata, Equatorial Guinea.
Historia imejirudia kwa Tembo kuwafunga Black Stars kwa penalti katiak fainali kama ilivyokuwa mwaka 1992 walipotwaa taji lao la kwanza.
Shujaa wa Ivory Coast leo aliuwa kipa wao Boubakar Barry aliefunga penalti ya mwisho akitoka kuokoa mkwaju wa kipa mwenzake Razak Braimah na kumaliza kiu ya miaka 23 ya kutotwaa ubingwa wa taji hilo.
![]() |
Rais wa Equatorial Guinea Teodoro Obiang na Rais wa FIFA Sepp Blatter awali walikuwepo uwanjani kukagua vikosi na baadaye kugawa medali na kombe kwa mshindi.
Post a Comment