0




 Alisema nchi hio ingeweza kutengeza mtambo wa kisiri wa nuklia chini ya ardhi kuisiaidia kurutubisha madini ya Plutonium.

Aliongeza kwamba pia angeisaidia Venezuela kuzalisha kawi ya nuklia.
Bwana Mascheroni alifanya kazi kwa karibu miaka kumi katika kitengo cha kutengeza zana za nuklia katika mahabara ya kitaifa ya Marekani ambako bomu la kwanza la Atomiki lilitengezwa.
Mkewe alikuwa mwandishi wa maswala ya teknolojia katika mahabara hio.
Aliachishwa kazi mwaka 1988
Katika mahojiano na shirika la habari la AP, alisema alifanya mawasiliano na nchi nyingine baada ya wazo lake la kutengeza kawi safi ya nuklia kukataliwa na maafisa wa baraza la Congress.
Mascheroni alisema alifanya mazungumzo na Venezuela, baada ya Marekani kukata wazo lake la kuzalisha kawi safi ya nuklia.
Serikali ya Marekani,imesema kuwa haiamini kuwa Venezuela ilikuwa inajaribu kuiba siri zake za kutengeza zana za nuklia.


Post a Comment

 
Top