0





Kikao cha Bunge la Tanzania leo kimevurugika kutokana na vurugu za baadhi ya wabunge waliokuwa wakibishana kuhusu swala la kiongozi wa chama cha upinzani Profesa Ibrahim Lipumba wa chama cha CUF kushambuliwa na polisi jana kwa madai kuwa alihusika katika maandamano kinyume cha sheria.


Hoja iliamshwa na mbunge ambaye pia ni kiongozi wa upinzani, James Mbatia, aliyetaka swala hilo lijadiliwe kwa dharura.

Hayo yametokea huku Profesa Lipumba akifikishwa mahakamani kusomewa mashtaka ya jinai. Regina Mziwanda anasimulia kutoka Dar Es Salaam.



Post a Comment

 
Top