Kwa miaka mingi tumekuwa tukisoma au kusikia
kuhusu wanyama ambao wanazaliwa na maumbile yasiyo ya kawaida na yamezua
hisia na imani tofauti kutoka kwa makundi tofauti
Kwa jamii fulani, wanyama
hao wanakisiwa kuwa na bahati mbaya au laana na kwa wengine ni ishara
kuwa jamii hiyo itakumbwa na maafa au janga.
Kwa wengine ni dalili
ya mwisho wa dunia na kwa dini zingine ni ishara kutoka kwa mungu
kuhusu dhambi za wanazotenda na hivyo wanaichukulia kuwa onyo kuhusu
jinsi adhabu yake itakavyokuwa kali.
Wanasayansi nao wanasema ni
mabadiliko ya vinasaba au Genes yanayosababishwa na magongwa au
mabadiliko ya hali ya hewa. Mwandishi wetu Robert Kiptoo alizuru shamba
moja mjini KitaleMagharibi mwa Kenya ambako wanyama hawa wenye ulemavu
wanatunzwa
Post a Comment