![]() |
Utafiti unafanyiwa sampuli nyingi za damu kuona ambavyo virusi hivyo vinaweza kuangamizwa |
Wanasayansi wanaokabiliana na janga
la Ebola nchini Guinea wanasema kwamba virusi vinavyosababisha ugonjwa
huo vimeanza kujibadilisha umbo na kuwa sugu hali inayoifanya vigumu
kutibu ugonjwa wa
Ebola.
Jambo hili linashuhudiwa kwa mara ya kwanza tangu tangu ugonjwa huo kugunduliwa mwezi Machi mwaka jana.Watafiti katika taasisi ya Pasteur mjini Paris Ufaransa, wamekuwa wakichunguza mamia za sampuli za damu kujaribu kubuni mbinu za kupambana na virusi hivyo.
Kwa sasa wanajaribu kubaini ikiwa kujibaidili kwa umbo virusi hivyo, kutasababisha maambukizi zaidi na ikiwa wanaweza kufanya lolote kuhusu ambavyo ugonwja huo unapimwa mwilini na pia ambavyo madawa yanatumika mwilini kupambana na ugonjwa huo.
Pia wanataka kuchunguza na kufanyia utafiiti chanjo dhidi ya ugonjwa huo.
Ugonjwa wa Ebola umewaua watu ziadi ya elfu nane huko magharibi mwa Afrika, wengi kutoka Guinea , Sierra Leone na Liberia
Post a Comment